Abdullah bin Abbaas Akishinda pamoja na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) usiku ili ajifunze swalah ya Tahajjud ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)

Mjomba wake Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu), alitamani mtoto wake Abdullah bin ‘Abbaas (Radhiyallahu ‘anhuma) ashinde na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) usiku ili afaidike na ushirika wake uliobarikiwa.

Katika riwaya ya Muslim na Tahaawi, Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anataja kwamba baba yake, Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuagiza kushinda usiku na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) nyumbani kwa shangazi yake Maimoonah. (Radhiya Allaahu ‘anha) ili kutazama na kujifunza jinsi Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) angetekeleza swala yake ya tahajjud. Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimwambia mwanawe Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu), ajifunze namna Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) anavyotekeleza swala yake ya tahajjud na kumfahamisha kuhusiana na hilo (ili aweze kuswali tahajjud kwa mujibu wa sunna).

Ibnu Abbas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anaeleza:

“Nilikaa nyumbani kwa shangazi yangu Maimoonah (Radhiya Allaahu ‘anha) ili nikachunguze tahajjud ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliamka usiku na akaenda kujisaidia. Kisha akanawa uso na mikono na kurudi kulala.

“Baada ya hapo aliamka tena na kuuendea mfuko wa maji wa ngozi, akafungua kamba ili kuruhusu maji yatoke kisha akafanya wudhu, huku akifanya udhu bila ya kutumia maji mengi, bali alifanya wudhu kamili, baada ya hapo akaanza kuswali.

“Niliamka na kisha nikaudhu. Baada ya hapo, nikasimama karibu na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) upande wake wa kushoto (kuungana naye katika Swalaah). Wakati wa kuswali, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kwa mkono wake mmoja, alinishika nyuma ya sikio, akanisogeza kwa upole upande wake wa kulia.

“Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliswali rakaa kumi na tatu usiku huo.

‘Ewe Mwenyezi Mungu! nijalie na nuru moyoni, nuru mbele yangu, nuru katika kusikia kwangu, nuru upande wa kulia kwangu, nuru upande wa kushoto kwangu, nuru juu yangu, nuru chini yangu, nuru mbele yangu, nuru nyuma yangu, na nipe nuru (katika kila ninachofanya).”

(Swahih Bukhaari #6316, Swahih Muslim #763 & Sharhu Maanil Aathaar #1702)

Check Also

Kachitidwe ka Mu’aaz (radhiyallahu ‘anhu) Kuwerenga Quraan Majeed pa Tahajjud

Mtumiki (swallallahu ‘alaihi wasallam) anatumiza Mu’aaz (radhwiyallahu ‘anhu) kuti akalamulire gawo lina la Yemen, ndipo …